Hizi ndio faida za kumkumbatia mumeo/mkeo
Umewahi kufikiria faida zinazopatikana kwa kumkumbatia mkeo mkiwa mmelala? Famasia yako ya Ndoa Maridhawa inakuletea faida 6 za kukumbatiana kitandani: 1. HUPUNGUZA SHINIKIZO LA KISAIKOLOJIA: Unapomkumbatia mkeo mkiwa mmelala husaidia kuzalisha kichocheo (homoni) cha furaha kiitwacho oxytocin. Homoni hii hufanya kazi ya kupunguza hatari ya kupatwa na maradhi ya moyo na kupunguza shinikizo la kisaikolojia. Hilo pia hupelekea kupunguza hatari ya kupatwa na maumivu ya kichwa na maradhi mengine. 2. USINGIZI MARIDHAWA: Wanandoa wanapokumbatiana husaidia kulala vizuri. Tafiti mpya zimeonesha kuwa kumbatio hupunguza cortisol na hivyo kupunguza shinikizo la kisaikolojia. Pindi cortisol inapopungua mwilini, moja kwa moja usingizi huwa mzuri na mwanana. 3. Unapomkumbatia inaweza kusababisha raha, hasa mambo yanapofikia kwenye hatua ya kucheza, lakini kabla ya hapo furahia ladha ya mgusano wa ngozi zenu kabla ya kusonga mbele… Moyo wako unatakiwa kuuhudhurisha katika eneo na muda wa mgusano hu...