Yajue mambo ambayo humpa furaha mpenzi wako
Uhusiano maridhawa katika ndoa ni kitu kinachohitaji kujituma kwa bidii kubwa. Ni kitu kinachohitaji subira, uelewa na upendo kwa pande zote mbili. Wakati unapenda kumfanya mwenzio kuwa mwenye furaha, kuna mambo kadhaa unayoweza kuyafanya kuhakikisha nawe unapata furaha. Ukweli kama hutofanya mambo haya matano, hutokuwa na zana sahihi zinazokupa furaha katika maisha ya ndoa yako: 1. Kumuamini. Imani ni ufunguo wa furaha katika maisha ya ndoa. Usipomuamini mwenza wako utaendelea kukosa utulivu na kuwaza kuwa yuko wapi, yuko na nani au anafanya nini. Stress na mashaka utakayoyapata kutokana na wasiwasi na hisia za kuhisi kile anachofanya vitakuondolea furaha yako. Ili uwe na furaha unatakiwa kuwa na imani, kumuamini. Imani inaweza kuchukua muda mrefu kuijenga, lakini ni kitu nyeti sana. Hakikisha unamweleza mwenzako wasiwasi wako pindi jambo fulani linapokuwa haliko sawa. Inaweza ikawa ni kutoelewa tu, lakini ukiiruhusu shaka ishike hatamu, inaweza kugeuka kuwa tatizo kubwa zaid...